Idara ya biashara ina kazi zifuatazo kama zilivyoanishwa katika sheria mama ya biashara.
1. Kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya uundwaji, uendelezaji, usimamizi na utekelezaji wa sera za biashara na mikakati yake.
2. Kutekeleza sheria na sera zinazohusiana na biashara Zanzibar.
3. Kuhamasisha (kukuza) masoko ya ndani, ya kikanda na kimataifa.
4. Kushirikiana na Taasisi nyengine katika masuala ya uzalishaji, uingizaji wa bidhaa kutoka nje na kutoa huduma.
5. Kutafuta na kutoa taarifa za biashara zinazohusiana na mauzo, manunuzi ya mahitaji ya biadhaa mbali mbali kwa watumiaji pamoja na kuishauri Serikali, jumuiya za biashara pamoja na wafanyabiashara mmoja mmoja. .
6. Kusimamia biashara za ndani, za kikanda na kimataifa na kutoa elimu na uwelewa unaofaa katika ukuzaji wa Biashara.
7. Kuweka mazingira bora (mazuri) kwa kuanzisha Public Private Partneship hususan katika mipango, utekelezaji na usimamizi wa agro processing initiatives kwa bidhaa za kilimo.
8. Kukuza business interprises zikiwemo wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs) na kuhimiza ukuaji na uongezaji wa faida katika mauzo ya biashara za ndani, kikanda na kimataifa.
9. Kufuatilia na kutathmini mfumo wa biashara na ufafanuzi wake.
10. Kufanya tafiti za masoko, survey na ufuatiliaji.
11. Kuratibu na kushiriki maonesho ya biashara, misafara ya biashara pamoja na matamasha ya biashara ya ndani na nje..
12. Kuweka njia au mfumo muafaka kwa wazanzibari kuchukua nafasi katika biashara za kimataifa na kushiriki kikamilifu katika maonesho ya biashara ya kimataifa.
13. Kuratibu na kushiriki maonesho na matamasha ya kimataifa ya biashara.
14. Kutayarisha na kutoa ripoti ya mwaka ya biashara.