IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI
UTANGULIZI
IIdara ya Mipang, Sera na Utafiti ni miongoni mwa Idara muhimu iliyo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.
Idara hii husimamia uandaaji wa Sera na Tafiti mbalimbali za Wizara, husimamia utekelezaji wa shughuli zinazofanywa na Idara/Taasisi nyengine zilizo chini ya Wizara, hali kadhalika ni Idara inayoratibu shughuli tofauti zinazohusu Wizara kwa Idara na Taasisi zote
Idara inafatilia kwa karibu shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Idara/Taasisi za Wizara hii ni pamoja na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi hiyo. Idara imeweza kusimamia shughuli za uandaaji na utekeelezaji wa kazi za Wizara, imeweza kusimamia uandaaji wa Mipango Kazi ya Idara na Taasisi nyengine, Hali kadhalika Idara imesimamia uandaaji wa bajeti kwa Wizara nzima.

