IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

UTANGULIZI

IIdara ya Mipang, Sera na Utafiti ni miongoni mwa Idara muhimu iliyo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.

Idara hii husimamia uandaaji wa Sera na Tafiti mbalimbali za Wizara, husimamia utekelezaji wa shughuli zinazofanywa na Idara/Taasisi nyengine zilizo chini ya Wizara, hali kadhalika ni Idara inayoratibu shughuli tofauti zinazohusu Wizara kwa Idara na Taasisi zote

Idara inafatilia kwa karibu shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Idara/Taasisi za Wizara hii ni pamoja na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi hiyo. Idara imeweza kusimamia shughuli za uandaaji na utekeelezaji wa kazi za Wizara, imeweza kusimamia uandaaji wa Mipango Kazi ya Idara na Taasisi nyengine, Hali kadhalika Idara imesimamia uandaaji wa bajeti kwa Wizara nzima.

SHUGHULI ZINAZOSIMAMIWA NA IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI.

1. Uandaaji na uibuaji wa Sera na Tafiti za Wizara.
2. Uandaaji na Utekelezaji wa Mipango ya Wizara.
3. Usimamizi wa Takwimu za Biashara na Viwanda.

Katika utekelezaji wa shughuli zake Idara imegawika katika vitengo vidogovidogo vitano. Ambavyo ni:-

1. Kitengo cha maendeleo ya Sera.
2. Kitengo cha kusimamia Utafiti..
3. bb;Kitengo cha ufuatiliaji na Tathmini.
4. Kitengo cha Takwimu.
5. Kitengo cha Mipango ya Wizara.

IDARA INA MAJUKUMU YAFUATAYO

1. Kuandaa mpango wa mwaka na mpango Mkakati wa maendeleo wa muda wa kati wa Wizara.
2. Kufuatilia, kukusanya na kuratibu mipango ya maendeleo ya Wizara.
3. Kusimamia, kufanya mapitio na tathmini ya sera, mipango, program na miradi.
4.  Kufanya tafiti na uchambuzi wa utekelezaji wa mipango, miradi na program mbali mbali na kutayarisha maelezo ya kisera kutokana na tafiti hizo;.
5.  v. Kutayarisha mfumo na muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripoti za utekelezaji.
6.  vi. Kuratibu uwanzishwaji na utekelezwaji wa mkakati wa mawasiliano ya habari.
7. Kutunza kumbukumbu za matumizi ya mifumo ya kompyuta;.
8. Kuratibu shughuli zote zinazohusiana na masuala mtambuka kama vile UKIMWI, jinsia, na mazingira.
9. Kuratibu Mpango wa kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini katika Sekta za Biashara na Viwanda – MKUZA.