IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

Majukumu Majukumu ya Idara hii ni kuziwezesha Idara kufanyakazi zake vizuri kwa kutoa huduma za kiutumishi kama vile kushughulikia ajira, uendelezaji rasilimali watu na uelimishaji, maslahi ya watumishi. Aidha Idara inatunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za rasilimali watu na kutoa huduma za kiutawala ili kuhakikisha mazingira mazuri ya kufanya kazi.